April 20, 2017Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wataanza tena mazoezi leo kuendelea na maandalizi ya michuano ya Kombe la FA na Ligi Kuu Bara.

Wachezaji Yanga walipewa mapumziko baada ya kutoka Algeria ambako waling’olewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

Yanga walifungwa mabao 4-0 mjini Algiers na kutolewa kwa jumla ya 4-1 kwa kuwa Dar es Salaam, Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Imeelezwa Yanga wataanza mazoezi kwenye Uwanja wa Polisi jijini Dar es Salaam kujiweka sawa na mechi zilizobaki za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV