April 20, 2017


Bondia Anthony Joshua ameendelea kuonyesha yuko siriaz katika maandalizi yake katika pambano dhidi ya  Wladimir Klitschko lililopangwa kufanyika Aprili 29, mwaka huu.

Klitschko yeye ameweka kambi nchini Austria pia akiendelea na maandalizi makali.

Lakini Joshua ameonekana ni mwenye tabasamu akilisubiri kwa hamu pambano hilo kwenye Uwanja wa wembley jijini London.

Kumekuwa na mijadala mingi kuhusiana na mabondia hao mmoja akionekana ni mkongwe sana na mwingine kijana sana. Lakini majibu yatapatikana ulingoni siku hiyo Joshua atakapopanda akiwa na rekodi yake ya kutopoteza hata pambano moja.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV