April 27, 2017Nahodha wa Azam FC, John Bocco ameendelea na mazoezi na wenzake na sasa anaonekana yuko tayari kwa mechi ya Jumamosi dhidi ya Simba.

Simba na Azam FC zitakutana Jumamosi katika mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tokea Bocco ameungana na wenzake baada ya kufanya mazoezi chini ya uangalizi wa daktari amekuwa akionekana kuimarika zaidi na sasa anashiriki mazoezi akionyesha keshokutwa, atakuwa mzigoni.


Nahodha huyo wa Azam FC, amekuwa gumzo kati ya wachezaji ambao mashabiki wengi wangependa kumuona akiwa uwanjani katika mechi hiyo.

Hivi karibuni, Bocco alipata bahati mbaya ya kuandamwa na majeraha mara kwa mara, hali iliyosababisha kukosa mechi kadhaa.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV