April 28, 2017




Wwale wababe waliowaondosha Yanga na Azam kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu, wamekutanishwa kwenye kundi moja katika michuano hiyo.

Yanga na Azam ndio waliokuwa wawakilishi wa Tanzania Bara kwenye michuano ya kimataifa msimu huu ambapo Yanga ilianzia Ligi ya Mabingwa Afrika, ilipoondoshwa na Zanaco ya Zambia kwenye hatua ya pili, wakadondokea Kombe la Shirikisho.

Ikiwa Kombe la Shirikisho ikaondoshwa na MC Alger ya Algeria, huku Azam katika michuano hiyo, ilianzia hatua ya pili na kukutana na Mbabane Swallows ya Swaziland na kuondoshwa kwa jumla ya mabao 3-1.

Katika ratiba ya hatua ya makundi iliyopangwa juzi Jumatano katika makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) jijini Cairo, Misri, MC Alger na Mbabane walipangwa Kundi B sambamba na timu za CS Sfaxien ya Tunisia na Platinum Stars ya Afrika Kusini.


Kundi A:  FUS Rabat ya Morocco, Club Africain (Tunisia), Rivers United (Nigeria) na KCCA (Uganda).

Kundi C: Zesco United (Zambia), Recreativo do Libolo (Angola), Al Hilal Elobeid (Sudan) na Smouha (Misri).


Kundi D: TP Mazembe (DR Congo), Supersport United (Afrika Kusini), Horoya AC (Guinea) na CF Mounana (Gabon).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic