Mshambuliaji nyota wa Chelsea, Diego Costa ameonekana akiwa na wakala maarufu wa kuuza wachezaji anayetambuliwa na Fifa, Jorge Mendes.
Mendes raia wa Ureno ndiye wakala wa Cristiano Ronaldo pia Jose Mourinho na alionekana akiwa na Costa na watu wengine wanane.
Kwa pamoja walikuwa katika mgahawa wa Kiitaliano wakila, kunywa na kufurahi pamoja.
Hali hiyo imezua maswali kuhusiana na Costa kuwa kama ataondoka na kwenda barani Asia hasa baada ya kuhusishwa na kwenda nchini China.
Lakini maswali ya kubaki Premier League na kujiunga na Man United pia yameonekana kutawala.
Hakuna aliyezungumza kwa kuwa mkutano huo wa siri umeripotiwa na gazeti la The Sun la England.
0 COMMENTS:
Post a Comment