Mshambuliaji nyota wa Chapecoense ya Brazil, Rossi amelambwa kadi nyekundu na kutolewa nje katika mechi ya Kombe la Liberatadores dhidi ya Club Nacional ya Uruguay.
Katika mechi hiyo, Nacional walikuwa nyumbani jijini Montevideo, Uruguay.
Rossi alitolewa nje kwa kulambwa kadi nyekundu baada ya kumshika makalio beki wa Club Nacional kama ambavyo beki Juma Nyosso akiwa Mbeya City alivyowahi kumfanyia Elius Maguri wa Simba wakati huo.
Chapecoense ni ile timu ya Brazil ambayo wachezaji wake walipoteza maisha kwenye ajali ya ndege hivi karibuni.
Kikosi cha Chapecoense, tayari kilikuwa kimelala kwa mabao 3-0 na Rossi aliona hakukuwa na ujanja zaidi ya kutumia njia za ziada.
0 COMMENTS:
Post a Comment