April 21, 2017
Mshambuliaji Mbwana Samatta, ameikosa kidogo tu Manchester United, jambo ambalo Watanzania wengi wapenda soka walitamani litokee.


Kikosi cha KRC Genk anayoichezea Samatta imeng’olewa kwenye michuanon ya Europa Cup hatua ya robo fainali, kwa kufungwa jumla ya mabao 4-2 na Celta Vigo ya Hispania.


Sasa Vigo ndiyo wamepangwa kukutana na Man United katika hatua ya nusu fainali na kama Genk wangevuka, maana yake wangekutana.Genk ililazimishwa sare ya bao 1-1 katika mechi ya nyumbani baada ya Celta Vigo kuwa imeshinda awali kwa mabao 3-2.

Inawezekana angevuka basi asingekutana na mshambulizi nyota Zlatan Ibrahimovic ambaye ameumia, lakini bado kukutana na Man United ilikuwa nafasi nzuri kwake.

Bado Samatta ana nafasi ya kuendelea kupambana kwa kuwa ana nafasi ya kuendelea kufanya vizuri na kujitangaza zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV