April 5, 2017
Salaam. Nathibitisha kuwa Kampuni ya Udalali ya Yono ambayo ni Wakala wa TRA imetangaza kuliachia gari mara moja basi  linalotumiwa  na wachezaji wa Serengeti Boys na wameomba nilifuate hata sasa, usiku huu.


Wamefuata amri ya TRA. Tutalifuata asubuhi, ili liendelee na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwapeleka vijana wetu Airport kuwahi ndege kwani vijana wetu wanatarajia kuondoka jioni.


Pia, TFF inampa pole nyingi Bw. Yono Kivella ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Njombe kwa msiba mkubwa uliompata. Inamtakia safari njema usiku huu na kuwahi mazishi ya mpendwa wake.

Alfred Lucas
MCO-TFF

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV