April 15, 2017



Pamoja na kuwa ndiyo amerejea, mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe amesema amepona na yupo fiti kimwili na kiakili kuichezea timu yake na kuiwezesha kupata ushindi dhidi ya MC Alger ya Algeria, leo Jumamosi.

Mchezo wa marudiano wa kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, utachezwa kwenye Uwanja wa Julai 5, 1962, mjini Algiers huko Algeria. Katika mchezo wa kwanza, Yanga ilishinda bao 1-0 jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa kwanza, Tambwe hakucheza kutokana na kuwa majeruhi wa goti, bao la Yanga lilifungwa na Thabani Kamusoko.

Tambwe raia wa Burundi alisema amejiandaa vizuri kuhakikisha wanaitoa MC Alger kwa ama kufunga au kutoa pasi ya bao. “Nipo fiti baada ya kutoka kuuguza jeraha la goti, nilikuwa na program yangu maalum ya mazoezi binafsi na sasa narejea uwanjani nikiwa fiti kabisa, kama sijafunga basi naweza kutoa pasi.

 “Tumejiandaa kushinda bila kujali nani atafunga bao, hiyo ndiyo nia yetu katika mchezo huu wa ugenini ambao ni muhimu kwetu na mashabiki wetu,” alisema Tambwe.


Tambwe alisema mechi ya awali dhidi ya MC Alger alikuwa ana uwezo wa kucheza, lakini alihofia kujitonesha kutokana na kutopata nafuu majeraha hayo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic