Wachezaji wa Yanga akiwemo Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, wanaelezwa kuachwa na ndege.
Imeelezwa wameachwa na ndege mjini Algiers nchini Algeria na hii inatokana na wao kushindwa kuendana na ratiba.
Kutokana na hali hiyo, wachezaji hao watabaki nchini humo hadi Jumatano.
Hata hivyo, imeelezwa kuna juhudi za kufanya waondoke mapema zaidi.
Yanga walikuwa nchini humo kucheza mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya MC Alger na walitandikwa mabao 4-0.
Kabla, wachezaji wa Yanga waliende Aligeria kwa makundi, wengine wakipitia Dubai na wengine Istanbul nchini Uturuki.

0 COMMENTS:
Post a Comment