April 3, 2017Miaka michache ijayo, huenda Jamaica ikawa na mwanariadha matata kabisa kama ilivyo kwa Usain Bolt.

Hata hivyo, mwanariadha huyo ni mwanadada na hiyo inatokana na binti wa miaka 12, kushinda katika mashinda ya shule kwa kuweka rekodi mpya ya dunia.


Brianna Lyston ameweka rekodi ya mbio za Mita 200 kwa mataifa ya Caribbean baada ya kumaliza kwa sekunde 23.72.

Rekodi hiyo ni ya Olimpiki na iliwahi kuwekwa na  Griffith-Joyner katika michezo ya mwaka 1988.

Brianna kutoka katika shule ya St Jago High ameweza kumaliza sekunde 0.88 kabla katika rekodi nyingine ya Oneika McAnnuff, jambo ambalo linaonyesha binti huyo ni hazina mpya.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV