April 19, 2017


Beki wa kati wa FC Barcelona, Gerard Pique ameonyesha wazi kupinga mwamuzi wa mechi ya Real Madrid Vs Bayern Munich kumtoa nje kwa kadi nyekundu kiungo Arturo Vidal.

Vidal alionekana kumchezea rafu Marco Asensio wa Madrid na kutolewa nje katika mechi ya pili ya robo fainali kati ya Madrid na Bayern waliokuwa wageni.

Bayern ilipoteza mechi hiyo kwa kufungwa mabao 4-2. Pique ameonyesha hisia zake na kusema kosa hilo la mwamuzi, ndiyo limeibeba Madrid.

Hata hivyo, ameonekana kueleza hisia zake kwa kitaalamu akitumia alama na desh tu.


Madrid na Barcelona ni wapinzani wakubwa nchini Hispania. Leo Barcelona wana kazi kubwa ya kuing’oa Juventus ambayo katika mechi ya kwanza iliwashinda kwa mabao 3-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV