April 19, 2017



Uongozi wa Klabu ya Simba imemtaka Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kujiuzulu kwenye nafasi yake hiyo na kubakia kama Mwenyekiti wa Soka wa Mkoa wa Kagera.


Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema kwamba kutokana na Malinzi kuwa na vyeo hivyo viwili kwa wakati mmoja ameshindwa kulitolea haki suala lao linaloendelea juu ya kupewa pointi tatu za timu ya Kagera ambayo inatokea mkoani kwake.


“Tunamtaka Malinzi ajiuzulu moja ya nafasi zake mbili anazishikiria ya Mwenyekiti wa Soka Kagera na urais wa TFF, kwani sasa ameshindwa kabisa kutolea haki juu ya pointi tatu ambazo tumepewa kutoka kwa timu ya Kagera Sugar ambayo inatoka mkoani kwake.



“Suala hilo kwa sasa linapindishwa wakati lipo wazi na hukumu yake ilishatoka lakini ameamuru kamati nyingine ikae tena na kuanza kulichunguza upya suala hilo,” alisema Manara.



Katika hatua nyingine Manara ameijia juu kamati inayosimamiwa na Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa ambayo imeliibua upya suala la Simba kupewa pointi na kamati ya Saa 72.



“Tumechoka na dhuruma ambazo tunazofanyiwa kila siku, baada ya kupewa pointi watu wanaibuka na kutaka iundwe kamati mpya kulichunguza suala letu wakati tayari Kamati ya Saa 72 ilishabaini kwamba Mohammed Fakhi ana kadi tatu za njano na hakustahili kucheza mechi yetu.


"Sasa mtu anaona halishishwi na hali hiyo anaibuka na kuanzisha kamati mpya kulichunguza suala letu.

“Unaunda kamati ambayo ndani yake ina mtu kutoka Kagera, Jonesia Rukyaa ambaye alishawahi kutunyonga huko nyuma na pia anatokea mkoa wa Kagera sasa hapo unatarajia itatokea nini kama siyo kunyimwa haki yetu.


“Niwaambie kwamba tumechoka kuendelea kuhujumiwa kila siku na kama hatutapata haki kwenye hili basi tunaweza kuandamana japo hatutaki tufanye hivyo, ila watu wachache wanashinikiza sisi tufanye mambo mabaya ambayo yatachafua sura ya soka letu kutokana na kushindwa kutupa haki yetu,” alisema mbele ya waandishi wa habari, leo.            

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic