April 21, 2017Beki wa kati wa Simba, Method Mwanjale leo amefikisha siku 69 tokea aumie na huenda ndiyo akakaa nje hadi mwisho wa msimu.

Mwanjale raia wa Zimbabwe, aliumia Februari 11, mwaka huu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons ya Mbaye kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Hadi sasa Mwanjale hajaanza mazoezi mepesi na Simba imebakiza mechi tatu tu za Ligi Kuu Bara kumaliza msimu.

Hii inaashiria hatakuwa fiti hata kama ataanza mazoezi wiki moja ijayo kutokana na hali ilivyo na kama akirudi, huenda mechi ya mwisho kabisa.


Mwanjale amekuwa tegemeo katika kikosi cha Simba katika suala la ulinzi hadi alipoumia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV