April 28, 2017



Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma, ameendelea kuivuruga timu hiyo na safari hii imeelezwa ameondoka nchini na kuelekea Afrika Kusini bila ya kutoa taarifa kwa uongozi.

Ngoma, hivi karibuni aliingia kwenye mtafaruku na viongozi, pia mashabiki wa timu hiyo akidai ana majeraha huku taarifa zikiwepo yupo fiti na amegoma kwa makusudi kucheza.

Mshambuliaji huyo, tayari amekosa michezo kadhaa ya Ligi Kuu Bara, Kombe la FA na ile ya kimataifa kutokana na majeraha ya goti, nyonga.

Kwa mujibu wa vyanzo mshambuliaji huyo ameondoka nchini mwenyewe na kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kujitibu majeraha hayo, lakini viongozi wanaonekana kutojua kwa ufasaha kuhusiana na hilo.

Mtoa taarifa huyo alisema Ngoma akiwa nchini humo atatumia gharama zake kwa ajili ya kujitibia licha ya kuwepo makundi mbalimbali ya mitandao ya WhatsApp waliokuwa wakichangishana kwa ajili ya kumtibia yeye na beki raia wa Togo, Vincent Bossou.

“Tumepata taarifa za Ngoma kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kwenda kujitibia majeraha ya goti na nyonga iliyokuwa inamsababishia azikose baadhi ya mechi za michuano ya kimataifa, ligi kuu na Kombe la FA.

“Tumesikia anakwenda kujigharamia mwenyewe matibabu yake wakati uongozi na baadhi ya mashabiki walikuwa wanachangishana kwa ajili ya kufanikisha matibabu yake huko Sauzi, hivyo tumeshangazwa na mshambuliaji huyo,” kilisema chanzo cha taarifa.

Alipotafutwa Meneja Mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh, kuzungumzia hilo, alisema: “Hizo taarifa ninazisikia kama wewe ulivyosikia, sina taarifa rasmi juu ya safari yako hiyo.”


Naye Daktari Mkuu wa Yanga, Edward Bavu alisema: "Sijapata taarifa rasmi za Ngoma kuondoka, nilizisikia taarifa hizo za kuondoka lakini hajaniambia na kama ameondoka basi alitakiwa aniambie, ngoja nifuatilie halafu nitakupa taarifa rasmi."

SOURCE: CHAMPIONI 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic