Kocha Mkuu wa MC Alger, Kamel Mouassa amesema moja ya njia ya kuikamata Yanga ilikuwa ni kuzuia winga zake pamoja na mabeki wa pembeni.
MC Alger imeifunga Yanga kwa mabao 4-0 katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho na kuing'oa kwa jumla ya mabao 4-1.
Kamel amesema Yanga hawakuwa na njia mbadala hata walipowafunga wao katika mechi ya kwanza zaidi ya mipira ya krosi.
“Yanga ni wazuri sana pembeni, ilikuwa ni lazima kupunguza makosa na kuzuia mipira ya pembeni.
“Lakini tulikubaliana kutafuta faulo nyingi karibu na lango lao kwa kuwa tuna wapigaji wazuri,” alisema akizungumza na mtandao wa mashabiki wa timu hiyo ambao pia wanatumia jina la Ultras.
“Baada ya Yanga kutakuwa na kazi ngumu zaidi mbele na ndiyo mpira ulivyo. Tunaomba muendelee kutuunga mkono zaidi.”
0 COMMENTS:
Post a Comment