Baada ya sare ya bila mabao dhidi ya Simba, Kocha Mkuu wa Toto African, Flugence Novatus amesema wameamsha matumaini ya kuendelea kupambana kubaki Ligi Kuu Bara.
Novatus amesema anaamini kikosi chake kilionyesha soka safi dhidi ya Simba na walipata nafasi nyingi zaidi ambazo hawakuzitumia.
“Kama tungezitumia tungepata pointi tatu. Imeshindikana, sasa tunaangalia mbele katika mechi zilizobaki,” alisema.
Toto African walionyesha soka safi katika mechi hiyo huku Simba walioonekana wangeshinda, wakishindwa kabisa kuonyesha cheche zao.
0 COMMENTS:
Post a Comment