April 17, 2017



Siku chache baada ya Azam kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya JKT Ruvu, Kocha wa Azam, Aristica Cioaba, raia wa Romania, amekiri kukutana na ushindani mkubwa kwenye michezo ya mwishoni mwa ligi kutokana na kutoshinda kwenye michezo mitatu mfululizo.

Kwenye michezo hiyo, Mromania huyo aliyechukua mikoba ya Mhispania, Zeben Hernandez katika kukinoa kikosi hicho, ameambulia sare mbili dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo hawakufungana, JKT Ruvu mabao 2-2 na kichapo kutoka kwa Yanga cha bao 1-0.

Aristica amesema kwamba ugumu huo kwa asilimia kubwa unachangiwa na kikosi chake kuandamwa na majeruhi wengi pamoja na timu ambazo wanacheza nazo kwa sasa kuhitaji matokeo zaidi kwa ajili ya kujiweka kwenye mazingira mazuri kwenye ligi.

“Utitiri wa majeruhi hasa wale wa kikosi cha kwanza ni miongoni mwa sababu za matokeo mabaya kwetu kwa sababu wale nyota wa kutumainiwa ndiyo tunakosa huduma zao na kunilazimu kuwatumia hawa wengine nilionao.

“Lakini pia hatufanyi vyema kwa sababu karibu mechi zetu zote tunacheza na watu wanaohitaji matokeo zaidi kuliko sisi ambao tunaelekeza nguvu zetu kwenye Kombe la Shirikisho (FA),” alisema.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic