April 2, 2017MPIRA UMEKWISHAAAAA
DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
Dk 88 nafasi nzuri kabisa kwa Kagera, Mbaraka anajichanganya, mpira unamkuta Mangoma anaachia mkwaju, hatari goal kick
Dk 87 Mavugo anaaachia mkwaju unapita juu kidogo
Dk 85, Bado inaonekana ni vigumu Simba kusawazisha kwa kuwa wanaonekana na haraka
Dk 83, mkwaju wa faulo anapiga Banda unawagonga mabeki na kuwa kona. Inachongwa, Kaseja anadaka vizuri kabisa hapa


SUB Dk 82, Ally Ramadhani anaingia upande wa Kagera kuchukua nafasi ya Ame Ali
Dk 82, Fakhi anaokoa na kuwa kona, Simba wanachonga na kuwa kona, inachongwa hapa Kazimoti anadhibitiwa na inaokolewa
SUB Dk 81, Simba wanamtoa Kichuya na nafasi yake kuchkuliwa na Mwinyi Kazimoto
Dk 81, Mo Ibra anaachia mkwaju mkali hapa lakini Kaseja anadaka kwa ufundi kabisa na kuutoa nje kwa kuwa Ame Ali yuko chini
Dk 80 sasa, Simba wanaonekana kuwa na papara katika mashambulizi yao
SUB Dk 76, mkongwe Themi Felix anaingia kuchukua nafasi ya Edo Christopher


Dk 74, kulikuwa na mchezaji wa Kagera anatibiwa, sasa ndiyo anatolewa nje hapa
Dk 71, Simba wanapata kona nyingine, inachongwa na Kichuya lakini Kagera wanaokoa hapa
Dk 69, Simba wanapata kona, Kichuya anaichonga inaokolewa na Matogolo na kuwa kona, inachongwa tena na Kaseja anadaka vizuri lakini kuna mchezaji wa Kagera anashika pale. Mwamuzi hakuona
Dk 67, Mavugo anapiga shuti sentimeta chache linapita juu
Dk 66 SUB Kagera wanamtoa Makarai anaingia Anthony Matogolo.

GOOOOOOOO Dk 61, Simba wanapata bao la kwanza baada ya shuti la Liuzio kutemwa na Kaseja na Muzamiru anaachia mkwaju unajaa wavuni
SUB Dk 58, Simba wanamtoa Ndemla na nafasi yake inachukuliwa na Liuzio
KADI DK 57, Mkude analambwa kadi ya njano kwa kuzozana na mwamuzi msaidizi
Dk 52 Simba wanafanya shambulizi jingine, lakini Fakhi anaokoa na kuwa kona. Kaseja yuko chini pale
Dk 50, kona safi ya Kichuya, Kaseja anaruka na kudaka vizuri kabisa
Dk 49 Kichuya anaachia mkwaju mkali kabisa, Kaseja anaokoa vizuri na kuwa kona. 
Dk 48, krosi nzuri ya Muzamiru lakini hakuna mtu hapa, Mavugo anajaribu kuuwahi lakiniGOOOOOOO Dk 45, Mechi inaanza kwa kasi na Edward Christopher anafunga bao safi kabisa kwa shuti kali baada ya mabeki wa Simba kuzubaa

MAPUMZIKODk 45+5 Simba wanapata faulo nje ya lango, Kichuya anachonga lakini anapaishaa buuuuuu
Dk 45+3 Banda anamtwanga ngumi mchezaji wa Kagera, lakini bahati yake mwamuzi hajaona kilichotokea, mpira unaendelea
Dk 45 sasa, Kaseja yuko chini akiendelewa kutibiwa baada ya kuokoa shuti la Banda


Dk 44, Banda anapanda akigongewa mpira, anafika ndani ya 18 anapiga shuti lakini Kaseja anapangua hapa
Dk 40, mpira wa adhabu wa Ajibu unatoka sentimeta chacge kwenye lango la Kagera
Dk 36 krosi nzuri kabisa ya Edo, Ame Ali Zungu anaruka na kupiga kichwa mbele ya Banda. Unatoka nje kidogooooo
Dk 34, Muzamiru anawageuza mabeki wa Kagera na kutoa pasi nzuri kwa Ajibu, anapaisha juuuuu
Dk 32, mpira umesimama kwa kwua kuna mchezaji wa Kagera anatibiwa


Dk 30, Bao hilo linaonekana kuanza kuwapa presha Simba ambao wanacheza haraka bila ya kuwa na umakini
GOOOOOOOO Dk 27, Mbaraka anageuka, nje ya 18, anaachia shuti kali kabisa na mpira unajaa wavuni 
Dk 25, Mavugo anapata nafasi lakini shuti lake linakuwa kuubwa
Dk 23, Kagera wanapata kona hapa baada ya Juuko kuutoa mpira, inachongwa hakuna kitu
Dk 21 Semvuni wa Kagera naye anajinyoosha lakini shuti lake linakuwa kuuuuubwaaaa
Dk 19, Ndemla anageuka na kuachia shuti kali lakini linatoka juu sentimeta chache


Dk 17 Ndemla katika nafasi nzuri anaachia shuti lakini Kaseja anaokoa na kuwa kona, inachongwa na Kichuya lakini wanaokoa
Dk 16, Mavugo anageuka na kuachia shuti kali kabisa lakini mpira unaokolewa na Fakhi
Dk 10 Zimbwe anafanya kosa kubwa kwa kupiga mpira mfupi wa kichwa lakini shuti la Mangoma linaokolewa na Agyei
Dk 8, Kichuya anaingia na kuachia shuti kali lakini goal kick
Dk 6, Simba wanaaanza kupanga mashambulizi upya lakini inaonekana Fakhi yuko vizuri


Dk 4 sasa, Kaseja yuko chini dakika ya pili akiwa anatibiwa. Inaonekana ni baada kupangua shuti la Ndemla
Dk 2, Ndemla anageuka na kuachia mkwaju mkali kabisa hapa, lakini Kaseja anaonyesha umahiri, anapangua kwa ufundi kabisa na kuwa kona
Dk 1, mpira umeanza taratiibu kila upande ukionekana unataka kufanya vizuri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV