April 2, 2017


Pamoja na Yanga kumuacha acheze mbele peke yake, Obrey Chirwa ndiye mchezaji aliyesumbua zaidi katika mechi ya jana, Yanga dhidi ya Azam FC.

Chirwa ndiye aliyefunga bao pekee katika mechi hiyo Yanga ikishinda kwa bao 1-0.

Pamoja na kwamba alikuwa pekee mbele na Yanga wakijilinda zaidi lakini Chirwa alikuwa bora kuliko washambulizi wote waliocheza mechi ya jana.

Kwani alifanikiwa kufanya kila plani iliyotakiwa na Kocha George Lwandamina.

Kwanza ilikuwa ni kukaa na mpira kuwasubiri wenzake, pili ilikuwa ni kuwapa presha mabeki wa Azam FC wasipande kusaidia mashambulizi, hasa wale wa kati pamoja na kiungo mkabaji, Himid Mao.

Lakini pia kuwatafutia kadi na wakati mwingine kutengeneza faulo ili kupunguza mashambulizi kwa Yanga.


Bao lake, ilikuwa ni pamoja moja tu kutoka kwa Haruna Niyonzima naye akafanikiwa kukatika katikati yao na kufunga akiwa ametulia kabisa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV