April 1, 2017MPIRA UMEKWISHAAAAAA....
KADI Dida analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda
-SUB Juma Mahadhi anaingia kuchukua nafasi ya Msuva


DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
Dk 89, Yanga wanaendelea kupoteza muda lakini wakipata nafasi wanazitumia vizuri lakini Aishi Manula anaonekana kuwa vizuri
Dk 86, Sure Boy ndani ya 18, anaachia shuti lakini goal kick
Dk 85, Himid anajaribu kuachia shuti hapa lakini linaonekana hali halina kasi
Dk 84, faulo inachongwa na Mwashiuya lakini haina kitu, anapiga juuuu

Dk 83, Yanga wanapata faulo nje ya lango la Azam FC, mpigaji akiwa mzuri, basi wanaweza kupata bao tena
Dk 80 sasa, Yanga wanaonekana kuupoza mpira huku Azam FC wakiwa wamejawa hofu wakitaka kusawazisha
SUB DK 77, Bruce Kangwa anaingia kuchukua nafasi ya Shabani
Dk 77, Sure Boy anaachia shuti kali hapa na mpira unambabatiza beki wa Yanga na kuwa kona
Dk 76, Yanga wanaingia vizuri, Chirwa anamgeuza Gardiel kama chapati lakini krosi yake inaokolewa na Yakubu
Dk 75, Yanga wamechangamka kwa sasa, wanakwenda vizuri na Mwashiuya na Martin wanaonekana kuwabana zaidi
Dk 74, Azam wanafanya shambulizi, Sure Boy anaachia mkwaju lakini Dida kama nyani anadaka 


GOOOOOOOO Dk 70, mabeki wa Azam FC walitegeana kati ya Amoah na Mohamed, Chirwa akaiwahi pasi ya Niyonzima na kuwaaadhibu kwa mkwaju mkali uliogonga mwamba wa juu na kujaa wavuni
Dk 70 Mpira unaonekana kupunguza kasi, lakini kila upande unacheza taratibu
SUB Dk 69, Anakwenda nje Singano na Joseph Mahundi anaingia kuongeza nguvu upande wa Azam FC
Dk 68, Chirwa anaunganisha krosi ya Juma Abdul lakini mpira unaishia mikononi mwa Dida
Dk 67, Bossou aliangushwa hapa, mwamuzi akapeta, naona amesimama kama vile anamshangaa


Dk 64, nafasi nzuri kabisa kwa Affur lakini alishindwa kulenga lango
Dk 62, Kona ya Singano kwenye lango la Yanga hapa, unaokolewa
Dk 61, shuti kali la Sure Boy linapita juu, lakini mwamuzi anasema kuna mchezaji aligusa, konaaa
Dk 60, Yanga wanagongeana vizuri na Mwinyi anaachia shuti kuuuubwa lisilo na manufaaa
KADI Dk 58, Gardiel analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Msuva aliyekuwa amemtoka 
Dk 57, Azam Fc wanapata kona ya sita ya mchezo wa leo. Inachongwana Himid Mao, Yanga wanaokoa 
Dk 55, mpira wa adhabu wa Singano unatoka nje kidogo juu ya lango la Yanga


SUB Dk 54, Anaingia Geofrey Mwashiuya kuchukua nafasi ya Deus Kaseke
KADI Dk 53 Cannavaro analambwa kadi ya njano baada ya kumuangusha Affur
Dk 51, Msuva anaingia vizuri na kuachia fatak, mpira unatoka sentimeta chache juu ya lango la Azam FC
KADI Dk 47, Sure Boy analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Martin
DK 46, krosi nzuri ndani ya lango la Yanga lakini Chilunda anaukosa mpira hatua chache kutoka lango la Yanga
Dk 45, Mpira umeanza ikionekana kila timu inataka kupata bao la mapema na kumaliza mchezo
SUB DK 45, Affur anaingia kuchukua nafasi ya Yahaya aliyeumiaMAPUMZIKO
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 45, krosi nzuri kabisa ya Haji Mwinyi kali hakuna mtu ndani ya eneo la Azam FC
Dk 44 sasa, Yahaya anatolewa nje baada ya kukaa chini kutokana na maumivu ikiwa ni mara ya tatu kwake katika mechi hii leo. Anatolewa nje tena na machela


Dk 43 tena, Sure Boy anaachia mkwaju mkali baada ya Bossou kuboronga, lakini goal kick
Dk 42, Singano anaachia shuti kali nje ya 18 lakini inakuwa goal kick
Dk 41, krosi safi ya Gardel, Yahaya anaachia shuti lakini Cannavaro anaweka mguu unakuwa wa kurusha
Dk 40, nafasi nyingine nzuri kwa Yanga lakini Msuva hakuwa makini, goal kick
Dk 38, Yaya anaingia, anaachia mkwaju mkali kabisa hapa lakini Dida anafanya kazi nzuri na kuokoa, inakuwa konaaaa, inachongwa na Himid, Dida kama kawa anadaka vizuri kabisa
Dk 36, Kaseke anaingia na kupiga krosi safi lakini Amoah anaosha mbali kabisa


Dk 34, Haji Mwinyi analazimika kutoa mpira na kuwa kona
Dk 33, Chirwa anaingia vizuri lakini Azam FC wanaokoa na kuwa konaaaa, inachongwa na Niyonzima lakini Aishi anadakakwa ulaini kabisa
Dk 33, Shaaban Iddi anajaribu kumtoka Bossou lakini anaokoa
Dk 31, krosi safi ya Gardiel, Sure Boy anaachia shuti lakini hakulenga lango
SUB Dk 30, Emmanuel Martin anaingia kuchukua nafasi ya Zulu ambaye ameumia
Dk 28, Zulu anatolewa nje akiwa kwenye machela baada ya kuumia huku akilia, inaonekana akilia kwa maumivu, lazima hataendelea


Dk 26 Zulu anaachia shuti kali kabisa hapa. Goal Kick, lakini yuko chini, atakuwa aligonga mguu wa HimidDk 23 Yanga wanajaribu kufanya shambulizi lakini hakukuwa na umakini
Dk 21, Himid Mao anamuangusha Msuva na kulambwa kadi
Dk 19 sasa, hakika Azam FC wanaonekana kutawala zaidi eneo la katikati wakifanya wanavyotaka. Yanga wanaonekana ni wapole na hakuna shambulizi kali wanalopeleka
KADI Dk 15, Bossou analambwa kadi ya njano kwa kumparamia Singano ambaye ametibiwa tayari
 Dk 12, Yahaya anaachia shuti kali lakini goal kick
Dk 11, Azam FC wanagongeana vizuri na kuingia kwenye lango la Yanga lakini Makapu anaokoa hatari
Dk 9, Gardiel anafanya kazi ya ziada kuokoa krosi ya Chirwa na kuwa konaaa. Inachongwa hapa lakini hakuna kitu


Dk 8, krosi safi ya Singano, Chilunda anaruka na kupiga kichwa lakini Cannavaro anaokoa tena
Dk 6, Dida analazimika kuwahi kutoka na kuokoa mpira mikononi mwa Sure Boy
Dk 5, basi nzuri ya Msuva lakini Juma Abdul anashindwa kuuwahi
Dk 3, Cannavaro anafanya kazi ya ziada, analala na kuokoa, kona. Inachongwa na Singano, Yanga wanaokoa vizuri
Dk 2, Azam FC wanaonekana kugongeana vizuri katika eneo la kati ya uwanja, lakini hakuna mamdhahara kwenye lango la timu yoyote
DK 1, mechi imeanza taratibu huku kila upande ukionekana haujatulia vizuriTAKWIMU
Kabla ya mechi hii, Yanga na Azam FC zimekutana mara 17. Mechi ya leo inakuwa mechi ya 18 tokea zilipoanza kukutana kwa mara ya kwanza msimu wa 2008-09.

Kati ya hizo, rekodi zinaonyesha hivi;

Yanga IMESHINDA 5
Azam FC IMESHINDA 5
SARE 7

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV