April 7, 2017


Wawakilishi wa Tanzania michuano ya kimataifa, Yanga wameingia kambini kwa ajili ya maandalizi yao ya mwisho dhidi ya MC Alger ya Algeria, Jumamosi.

Yanga watakuwa wenyeji wa waarabu hao Jumamosi na imeelezwa wataweka kambi kwenye Baraza la Maaskofu eneo la Kurasini jijini Dar es Salaam.

“Kambi ambayo imekamilika ilikuwa ni ile ya kule kwenye Baraza la Maaskofu, Kurasini. Sasa kama kutakuwa na mabadiliko, ntawajuza,” kilieleza chanzo.

Imeelezwa Yanga wameamua kuweka kambi huko kutokana na utulivu wa eneo hilo lakini pia ulinzi wa uhakika katika eneo hilo.


Kikosi hicho kitakuwa kinafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV