Na Hussein Jani, Mwanza
Baada ya sare ya bila kufungana dhidi ya Toto Africans, jana. Mashabiki wa Simba wamewataka wachezaji wao “kukaza” katika mechi zilizobaki.
Mashabiki wa Simba mjini hapa, wameonyeshwa kukerwa na sar ya bila kufungana dhidi ya Toto kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jana.
“Kweli mimi sijafurahia, hasa ukiangalia timu haikucheza vizuri. Haikuonyesha kiwango tunachotarajia, mechi tatu zijazo ni kipimo cha mwisho kwao,” alisema Daud Masanja mkazi wa Igoma.
Mwinshehe Ally ambaye alisema ametokea mkoani Shinyanga kuja hapa kuangalia mechi hiyo alisema:
“Unajua hata Mbao walituzidi kiwango, Toto nao pia. Nafikiri kuna sababu ya wachezaji kubadilika katika mechi tatu za mwisho.”
Mama Maghembe ambaye ni mkazi wa Kirumba karibu kabisa na uwanja huo, alisema mashabiki hawajafurahishwa sana na Simba lakini mechi tatu za mwisho lazima “wakaze”.
“Kweli wakaze, nasema wakaze kweli maana wengine Simba ikipotea tunaumia sana. Ubingwa umekaribia lakini wao hawaonyeshi kabisa kama wanataka kufanya vizuri. Naumia sana tena sana.”
Toto African ndiyo walionyesha kiwango kizuri zaidi ya Simba hasa katika suala la kupeleka mashambulizi mengi.
0 COMMENTS:
Post a Comment