April 16, 2017



Pamoja na Simba kupata sare ya bila kufungana dhidi ya Toto Africans, Msemaji wa Simba anaamini bado Simba ina nafasi ya kubeba ubingwa kwa kuwa iko kileleni kwa tofauti ya pointi sita.

Simba imefikisha pointi 62 na Yanga inafuatia ikiwa na pointi 56, hata hivyo Simba imecheza mechi 27 na Yanga ina pungufu miwili kwa kucheza 25.


Manara amesema: “Aliyenacho mkononi ni tofauti na anayesubiri kupata. Tuko kileleni kwa tofauti ya pointi sita, tusubiri kinachokuja. Ila niwaambie, nguvu za ubingwa ziko palepale.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic