Akufukuzaye, hakuambii toka. Lakini kwa Kocha, Arsene Wenger inaonekana imezidi kupita kiasi. Maana sasa mashabiki wa Arsenal wameamua kutembeza matangazo mtaani.
Baadhi ya mashabiki wa Arsenal wamekodi gari la matangazo lenye ujumbe unaoonyesha umefika wakati wa Wenger kuwaachia timu yao.
Mashabiki hao wanasisitiza Wenger aachie ngazi kwa kuwa wamechoka katokana na mwenendo wake.
Kama hiyo haitoshi, mashabiki hao wanaendelea kusisitiza wamekuwa wakisubiri mafanikio ya kubeba angalau ubingwa barani Ulaya, sasa ni mwaka wa 20 lakini hakuna mafanikio.
Hasira za mashabiki hao zimeamka zaidi baada ya Wenger kuonekana anataka kuongeza muda na yuko katika hatua za mwisho kusaini tena mkataba.
0 COMMENTS:
Post a Comment