April 17, 2017



Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, raia wa Cameroon, ameweka bayana kwamba mipango yake haijaharibika kabisa baada ya kuambulia pointi saba badala ya tisa ambazo walikuwa wanazitegemea kuzivuna kwenye michezo yao ya Kanda ya Ziwa.

Juzi Jumamosi Simba ilimaliza michezo yake ya Kanda ya Ziwa kwa kucheza na Toto Africans katika Uwanja wa Kirumba, Mwanza ambapo timu hizo hazikufungana. Kwenye mechi nyingine za ukanda huo Simba iliwafunga Mbao mabao 3-2 na kupewa pointi za Kagera Sugar licha ya kufungwa mabao 2-1 baada ya kumkatia rufaa beki Mohammed Fakhi ambaye alikuwa na kadi tatu za njano.

Omog alisema pointi ambazo wamepata Kanda ya Ziwa, zitaweza kuwasaidia kwenye kampeni yao ya kuchukua ubingwa.

“Siyo vibaya kwamba tumepata pointi saba badala ya tisa kama tulivyopanga awali, nasema hivyo kwa sababu ni bora tumeambulia pointi hizo kuliko tungefungwa kabisa kwani ingetutoa kwenye reli ya kugombania ubingwa.


“Ni ngumu kupata pointi hizo kwenye michezo hii ya mwishoni kwa sababu kila timu inakuwa inajipanga kikamilifu kuhakikisha haipotezi pointi kirahisi ili kujiepusha na suala la kushuka daraja,” alisema Omog.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic