April 28, 2017



Mwanariadha nyota nchini, Alphonce Simbu aliyeshika nafasi ya tano katika mashindano ya London Marathon, jana Alhamisi alitembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata mwaliko maalum wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harryson Mwakyembe.

Akizungumzia mwaliko huo, Simbu amesema: “Nimefurahi sana kupata mwaliko huu kwani inaonyesha ni kwa kiasi gani serikali inafanya jitihada za kutambua jitihada tunazofanya vijana wao katika kuliletea taifa sifa.”

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania ambao ndiyo wadhamini wakuu wa mwanariadha huyo kupitia king'amuzi chao cha DSTV, Johnson Mshana, amesema kuwa mwaliko huo unatoa picha kwamba serikali ipo karibu na watu wake, lakini pia itaimarisha kuendeleza michezo hapa nchini.

Multichoice Tanzania kupitia DSTV, imekuwa ikimdhamini Simbu tangu mwaka jana na udhamini huo pia umewanufaisha wanariadha wengine ambao wamekuwa kambini kwa muda sasa pamoja na Simbu.


Alphonce Simbu, ambaye pia ni mshindi wa medali ya dhahabu katika mashindano ya Mumbai Marathon yaliyofanyika mwanzoni mwa mwaka huu nchini India, ni miongoni mwa wanariadha wa timu ya Taifa itakayoshiriki mashindano ya dunia yatakayofanyika jijini London, Agosti, mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic