April 3, 2017


Timu ya taifa ya vijana wa Ghana chini ya miaka 17, wameonyesha wametokea katika nchi ya soka. Lakini vijana wa Tanzania, Serengeti Boys wakaonyesha wanajua zaidi kwa kuwa wako katika nchi ya vipaji.

Mechi ya kirafiki ya kimataifa ya timu hizo mbili imeisha kwa sare ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.


Ghana walianza kupata mabao yao mapema kupitia Sulley Ibrahim kabla ya Arko Mensah kuongeza la pili.

Hadi dakika za nyongezwa zinaonyeshwa, Serengeti ilikuwa nyuma kwa mabao mawili. 

Lakini dakika ya 90+5, mshambuliaji hatari wa Boys, Assad Juma akafunga bao la mkwaju wa penalti baada ya beki wa Ghana kunawa enero la hatari.

Dakika ya 90+10,  Muhsin Malima akavunja mtego wa kuotea na kumalizia kazi nzuri ya kiungo wao.



Bao hilo liliamisha shamrashamra uwanjani hapo na ikaonyesha kweli Boys wanastahili kuchangiwa, wanastahili kuandaliwa ili wakafanye vizuri nchini Gabon katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic