April 28, 2017Inaonekana kama zoezi la ukarabati wa uwanja wa Namfua mjini Singida umekuwa ukienda kwa mwendo wa kobe jambo ambalo linaweza kuwakosesha uhondo mashabiki wa mkoa huo.

Mashabiki wa soka mkoani Singida wanaweza kukosa raha ya kushuhudia mechi za Ligi Kuu Bara wakati Singida United ikiwa imereja katika ligi hiyo.


Kocha Hans van der Pluijm, lazima atataka maandalizi ya uhakika na pia mechi kuchezwa katika eneo ambalo lina uhakika jambo ambalo linaweza kusababisha Singida united kuhama mkoani hapo.

Taarifa za ndani zimeeleza kwamba, Singida United wanaweza kuhamia katika mkoa mwingine wa Dodoma ambao upo kanda ya kati.

"Kocha anataka uwanja ambao timu inaweza kucheza soka safi, huenda mwanzo timu ikahamia Dodoma halafu baada ya ukarabati itarejea Singida," kilieleza chanzo.

Lakini taarifa zinaeleza juhudi za makusudi zimekuwa zikifanyika kuhakikisha Singida United inaanza mechi zake za Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Namfua.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV