April 14, 2017Mshambuliaji Muargentina, Paulo Dybala ndiye aliyepiga bao mbili wakati Juventus ikiitwanga Barcelona kwa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Tayari sasa gumzo limehamia katika viatu vyeusi ambavyo anavaa mchezaji huyo.

Swali limekuwa kwa mini anavaa viatu vyeusi tupu vikiwa na nembo yake binafsi?

Wapo ambao wameanza kuhusisha viatu hivyo na imani za kishirikina lakini hawaendi moja kwa moja katika suala hilo.

Lakini mjadala wa mitandaoni kwa Kiitaliano, unaonyesha Dyabala ni mtu wa dini sana kwa kuwa makuzi yake ni kutoka katika familia ya Kikristo, iliyoshiba imani ya dini hiyo.


Lakini baadhi ya vijana, wanaamini Dyabala ni mtu anayehusika na nguvu za giza na ndiyo maana anaamini sana vitu vyenye range nyeusi. Yeye amekuwa kimya na hajalizungumzia hilo.

NEMBO YA DYABALA

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV