April 14, 2017




Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya, amesema mechi ya kesho Jumamosi dhidi ya Toto Africans itakuwa ngumu lakini nia ni kupata ushindi na kuvuruga rekodi ya Toto kutofungwa na Simba ndani ya miaka saba kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

“Nimesikia Simba haijawahi kuifunga Toto kwa miaka saba katika Uwanja wa Kirumba, wachezaji kwa pamoja tumedhamiria kushinda mchezo huo.


“Yawezekana mchezo huo ukawa balaa kwa kuwa tumejipanga kupata matokeo mazuri kwa kuibuka na pointi tatu."

Toto ni moja ya timu zimekuwa zikiisumbua sana Simba na mara nyingi zimekuwa zikikutana katika mechi ya mzunguko wa pili ambayo huchezwa jijini Mwanza.

Mara nyingi, wakati zinakutana, Simba huwa inawania kubeba ubingwa na Toto ikipambana kujikomboa kuteremka daraja.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic