April 8, 2017Yanga leo saa 10:00 jioni itacheza mechi ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya MC Alger ya Algeria, katika kuhakikisha wanashinda Kocha George Lwandamina amewaandaa wachezaji wake kutumia zaidi mipira ya mbali kupata mabao.


Yanga inacheza mchezo huo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Zanaco ya Zambia kwa sare ya bao 1-1.Katika mazoezi ya Yanga juzi na jana, kwenye Uwanja wa Taifa, Lwandamina akiwa na wasaidizi wake, Juma Mwambusi na Noel Mwandila, waliandaa programu ya dakika 30 kwa wachezaji wa timu kupiga mashuti makali nje ya 18 huku wakirudia zaidi ya mara tatu.


Katika mazoezi ya Yanga, wachezaji walikuwa wakipiga mashuti kwa mipira iliyotengwa kabla ya Lwandamina kuwabadilishia zoezi kwa kuwataka wapige mashuti hayo baada ya kutuliza mpira kifuani.


Akizungumza kuhusu mazoezi hayo, Mwambusi alisema: “Kile tulichokuwa tunakifanya ni sehemu ya programu zetu kwa sababu katika mechi lolote linaweza kutokea, tunataka timu iwe imara.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV