April 8, 2017
Leo Jumamosi kuna mechi kadhaa za Ligi Kuu England, lakini hii inaingia kwenye historia ya aina yake.

West Ham United itakuwa inawavaa Swansea, kila timu ikiwa inapambana kuepuka kuteremka daraja.

Katika kila timu, moja ya wachezaji watakaokuwa wanapambana kuziokoa timu zap ni ndugu Andre Ayew wa West Ham United na Jordan Ayew wa Swansea.

Hawa wataongoza vita, kuizamisha timu ya mwenzake na kuikoa yake.

Andre, 27, ni kiungo wa pembeni wa West Ham na Jordan, 25, ni mshambuliaji wa Swansea.

Wote wawili ni watoto wa gwiji la soka Ghana na Afrika, Abeid Ayew maarufu kama Pele.

West Ham inaonekana kuwa na nafuu kidogo ikiwa katika nafasi ya 15 baada ya kujikusanyia pointi 33. Swansea iko nafasi ya 18, tayari kwenye hatari baada ya kufikisha pointi 28. Inahitaji ushindi kwa nguvu zote.


Kama Swansea itashinda maana yake itafikisha pointi 31, West Ham itabaki na 33, maana yake itakuwa imejisogeza kwenye mdomo wa kuteremka daraja. Hivyo itakuwa ni mechi ya kugombea “maisha” ya Premier League inayowahusisha ndugu wawili, kila mmoja akitakiwa kuwa mwokozi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV