April 7, 2017MC Alger ya Algeria wamewasili nchini salama usiku huu, tayari kwa mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi.

MC Alger wametua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kupokelewa na baadhi ya maofisa wa ubalozi wao nchini.


Yanga watakuwa wenyeji wa waarabu hao Jumamosi na imeelezwa wataweka kambi kwenye Baraza la Maaskofu eneo la Kurasini jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha MC Alger kimetua jijini Dar es Salaam na wachezaji wake wakionekana kujiamini tayari kwa mechi hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV