April 22, 2017Yanga imefanya mazoezi yake ya mwisho leo ikiwa ni maandalizi ya mwisho kabla ya kuivaa Prisons, kesho. Lakini mazoezi yake yalikuwa siriazi hasa.

Kiungo Haruna Niyonzima raia wa Rwanda na Kelvin Yondani walikuwa wakichuana hasa katika kukabana na kuchezesha timu.

Mara kadhaa ilionekana kila mmoja alitaka kushinda au kufanya vizuri katika kikosi chake, ushindani ambao uliwaambukiza wengine kama Thabani Kamusoko.

Katika mazoezi hayo ya leo, Yanga walichezea zaidi mpira na inaonekana ni kwa kuwa ni siku moja kabla ya mechi.

Yanga itaivaa Prisons katika mechi ya Kombe la Shirikisho, michuano inayodhamiwa na Azam Media.


Mechi hiyo ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV