April 22, 2017



Baada ya Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumfungia mechi mbili beki wa Simba, Abdi Banda ambapo tayari adhabu hiyo ameshaitumikia, beki huyo amesema hatarudia tena kosa hilo.

Aprili 2, mwaka huu, Banda aliingia matatizoni kwa kumpiga ngumi nahodha na beki wa Kagera Sugar, George Kavila kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba wakati timu hizo zikipambana.

Banda alipelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu kwa kosa hilo la kumpiga Kavila na kuadhibiwa kwa adhabu ambayo alishaitumikia kwani alisimamishwa kucheza mechi yoyote hadi suala lake litakaposhughulikiwa.

Akizungumza Banda alisema: “Namshukuru Mungu suala langu limeisha, nimekoma na kuna kitu nimejifunza maana nilijiona mkosefu kwa kujadiliwa na watu wengi.


“Sitarudia tena kitendo kama kile licha ya mchezo wa soka kuwa na majaribu mengi ambayo yanaweza kukufanya uchukue uamuzi wowote ule, nimejifunza na kuanzia sasa mimi ni mtu mwema.


 “Kusimamishwa mechi mbili hakukuniathiri kwa kuwa mimi ni mchezaji mkubwa ila ninachokiangalia hivi sasa ni kuisaidia timu yangu iweze kutwaa ubingwa.”

Hata hivyo, kanuni za ligi kuu zinaweka wazi kwamba mchezaji anayepigana au kupiga uwanjani anafungiwa kucheza mechi tatu au zaidi, habari kutoka kwenye kamati hiyo zinasema Banda aliomba msamaha.


“Pia tumeona Banda ni mtu muhimu katika kikosi cha Taifa Stars ambacho kina mechi hivi karibuni ndiyo maana ikawa hivi,” alisema mmoja wa maofisa wa TFF.

1 COMMENTS:

  1. safi kabisa Banda umeonyesha kukomaa vilivyo na huo ndo uanaume, wahenga walishasema "Haja ya mja kunena, uungwana ni vitendo". Mungu asaidie usirudie tena maana Tulikumiss sana washabiki wako Simba vs Mbao Fc!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic