May 15, 2017



Zacharia Hans Poppe, amereja Simba.

Uamuzi wa Hans Poppe kurejea Simba umetokana na mkutano uliofanyika hadi saa 9 usiku wa kuamkia leo.

Hans Poppe amethibitisha kurejea kwake kundini baada ya mkutano huo na viongozi.

Hans Poppe aliamua kujiondoa katika kamati ya utendaji ya Simba na akawa akawa ametoka kwenye kamati ya usajili aliyokuwa mwenyekiti.

Lakini kikao hicho hadi saa 9 alfajiri usiku wa kuamkia leo, kimemaliza suala hilo na Hans Poppe ameamua kurejea.


“Kweli tumekutana hadi saa 9 usiku, mwisho tumekubaliana na tumeyamaliza vizuri. Huu ni wakati wa kusonga mbele,” alisema Hans Poppe.

1 COMMENTS:

  1. tatizo la viongozi wetu masilahi kwanza, ukiona hivyo ujue nae kaahidiwa kupata kipande chake cha keki ya simba au vipi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic