May 20, 2017



Hata kama itaukosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, hesabu zikienda sawa basi Simba itachota fedha nyingi zaidi msimu huu kuliko Yanga inayotarajiwa kutangaza ubingwa wa ligi kuu leo.

Katika msimamo wa ligi kuu, Yanga wanaongoza wakiwa na pointi 68 wakifuatiwa na Simba wenye 65 huku zote zikiwa zimebakiza mchezo mmoja. Yeyote anaweza kuwa bingwa licha ya Yanga kuwa na nafasi kubwa.

Simba isipotwaa ubingwa wa ligi kuu, itapata Sh milioni 40 kama kifuta jasho wakati Yanga itapata Sh milioni 81, lakini Simba itapata fedha nyingine Sh milioni 50 endapo itatwaa ubingwa wa Kombe la FA.

Wikiendi ijayo Simba itacheza fainali ya Kombe la FA dhidi ya Mbao FC kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma na ikishinda itapata Sh milioni 50 ambapo jumla msimu huu itapata Sh milioni 90.

Hii ina maana kwamba, Yanga wenye nafasi kubwa ya kuwa mabingwa leo, msimu huu watakuwa wamepata Sh milioni 81 pekee za zawadi ya ubingwa wakati Simba itapata Sh milioni 90, ikiizidi Yanga Sh milioni tisa.

Mabingwa watetezi wa ligi kuu, Yanga wakiuchukua ubingwa huo katika msimu huu watakuwa wamefanya hivyo mara 27, chini ya nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ atakayeweka rekodi ya kubeba taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic