May 28, 2017Uongozi wa klabu ya Simba umesema hautazungumza lolote kuhusiana na rufaa yao waliyopeleka Fifa hadi watakapopata mawasiliano sahihi na shirikisho gilo.

Makamu Rais wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' amesema hawatazungumzia kuhusiana na barua za kuunda zinazosambaa mitandaoni hadi watakapopata ile sahihi kutoka Fifa.

"Sisi hatujapokea barua yoyote kutoka Fifa na tunaendelea kusubiri, matarajio yetu ni hivi karibuni kwa kuwa nao wanafanya kazi zao kwa kufuata utaratibu wao.

"Lakini wanaosambaza barua zisizo sahihi mitandaoni hatujui wanafanya hivyo kwa nini, wamfurahishe nani au kwa faida ipi. Lakini sisi tutaendelea kusubiri barua kutoka Fifa," alisema.

Jana, kumekuwa na barua zinazosambaa mitandaoni zikielezwa kuwa ni kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), ikieleza kwamba Kagera itabaki na pointi zake hivyo Yanga itaendelea kuwa bingwa.

Simba imekata rufaa kupinga Kagera Sugar kurejeshewa pointi tatu wakati inaamini na ina vidhibitisho kuwa beki Mohamed Fakhi ana kadi tatu za njano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV