May 28, 2017


Baada ya kuitwanga Mbao FC kwa mabao 2-1 na kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho, Simba kesho italipeleka kombe hilo bungeni.

Makamu Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema wanakwenda bungeni kumpeleka mwali huyo kesho.

“Kweli tumepata mwaliko, tutalipeleka kombe bungeni kesho asubuhi. Baada ya hapo, safari ya kurejea Dar es Salaam itaanza,” alisema.


Simba ilipata ushindi ndani ya dakika 120 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bila bao huku Mbao FC wakionyesha upinzani wa hali ya juu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic