May 16, 2017




Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Imani Madega amesimuliwa namna alivyopata msiba mkubwa wa kufiwa na mwanaye.

Mwanaye huyo anaitwa Omary Madega na amefariki baada ya kupata ajali akiwa anaendesha gari la Madega akijaribu kuwakimbia madereva bodaboda.

Omary anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 32, aliuawa wakati akiwakimbia bodaboda katika eneo la Chalinze mkoani Pwani akiwa anatumia gari la baba yake mdogo, Madega ambaye kitaalamu ni mwanasheria.

Akizungumza na Championi Jumatano, Madega aliyeonyesha masikitiko makubwa alisema gari lililosababisha ajali ni Mitsubushi Pajero, mali yake.

“Nina msiba mkubwa sana ndugu yangu. Nilisafiri kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze ambako nilipitiliza kwenye project yangu. Nikiwa huko gari lilisumbua.

“Nikamuita Omary ambaye ni mtoto wa kaka yangu aje alishughulikie. Alipofika pale alikuwa na fundi, akamchukua na mtu ambaye amekuwa akisimamia nyumba yangu ninapokuwa Dar es Salaam pamoja na Shamba Boy wangu.

“Wote wanne waliondoka kwenda kuifuata gari nilipoiacha. Walipofika haikuwa na tatizo kubwa, kawaida ikishapoa huwa inawaka, basi wakaichukua. Sasa si unajua vijana, wakaona waingie mtaani kidogo.

“Kama dakika 10 tokea waondoke, nikapigiwa simu kwamba Omary kagonga watu watatu pale sheli na inasemekama mmoja amepoteza maisha na alikuwa anabishana na madereva bodaboda. Mwisho aliondoa gari kasi kama akiendelea Dar es Salaam.

“Dakika 5 baadaye sijajua hata cha kufanya, nikapigiwa simu ile gari imepata ajali na Omary amefariki dunia pamoja na yule mtunza nyumba,” alisema Madega.


Kwa Mujibu Madega Omary amezikwa Jumapili, mtunza nyumba wake kazikwa juzi na mchungaji wake bado ana hali mbaya katika hospitali ya Tumbi kwa kuwa mguu wake umevunjika vibaya na unahitaji upasuaji.

SALEHJEMBE INATOA POLE KWA MADEGA NA FAMILIA YAKE KUTOKANA NA MSIBA HUO MKUBWA WALIOUPATA.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic