May 10, 2017


Timu anayoitumikia Mtanzania, Thomas Ulimwengu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki Ligi Kuu ya Sweden, imeonekana kuwa ni kibonde baada ya kuburuza mkia kutokana na kucheza mechi saba za ligi hiyo mpaka sasa.


Ulimwengu ambaye alijiunga na timu hiyo mwanzoni mwa mwaka huu baada ya mkataba wake na TP Mazembe kumalizika, mpaka sasa ameshindwa kucheza hata mechi moja kutokana na kufanyiwa upasuaji wa goti.

Katika ligi hiyo yenye timu 16, AFC Eskilstuna inaburuza mkia ikiwa na pointi tatu baada ya kucheza mechi saba ambazo wametoka sare tatu na kufungwa nne huku wakishindwa kupata ushindi hata kwenye mechi moja.


Kwa mujibu wa ligi hiyo, timu mbili za chini kwenye msimamo zitashuka daraja moja kwa moja, huku ile ya tatu kutoka chini itacheza mechi dhidi ya timu iliyoshika nafasi ya tatu kutoka Ligi Daraja la Kwanza, itakayoshinda ndiyo itacheza ligi kuu msimu ujao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV