May 10, 2017


Baada ya JKT Ruvu kuchezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Toto Africans ya Mwanza, kocha msaidizi wa timu hiyo, Azishi Kondo, amesalimu amri na kuongea kwa unyonge kwamba anasubiri kuona timu mbili zikiungana na timu yake kushuka daraja msimu huu.

JKT Ruvu baada ya kichapo hicho, imeshuka daraja ikiwa na pointi 23 huku ikibakiwa na michezo miwili ambayo hata ikishinda haiwezi kuwaokoa na janga hilo.

Kondo alisema kuwa japokuwa wameshashuka daraja, lakini hawatakubali kufungwa katika mechi zao mbili zilizobaki dhidi ya Majimaji na Ndanda FC.

“Sisi tushashuka daraja na msimu ujao tutacheza Ligi Daraja la Kwanza, kwa sasa tunasubiri kuona ni timu gani tutaungana nazo, lakini japokuwa tumeshashuka, hatutakubali kufungwa kwenye mechi zetu mbili zilizobaki.


“Sasa hivi tunajipanga kucheza na Majimaji katika uwanja wetu wa nyumbani wa Mkwakwani uliopo Tanga, kisha tunamalizia na Ndanda kule kwao kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona na mechi zote tunataka kuibuka na ushindi,” alisema Kondo.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic