May 27, 2017


Mashabiki wengi wa Simba wameonekana kujiamini kwenda katika mechi ya fainali inayopigwa leo.

Simba vs Mbao FC katika mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ndiyo mechi inasubiriwa zaidi hapa nchini na mashabiki wa Simba wamekuwa wakiranda mitaani na mabango yenye ujumbe tofauti.

Ujumbe ulio katika mapango hayo unaonyesha mashabiki wa Simba wanajiamini kuwa leo mwali ni wao na safari ya kushiriki michuano ya kimataifa, imewadia.


Hata hivyo, watalazimika kusubiri dakika 90 za mechi hiyo ili kupata uhakika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV