May 7, 2017
Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog amewataka wachezaji wake kuindoa presha ili wacheze mpira katika kiwango chao wakati wakiivaa Lyon katika mechi ya Ligi Kuu Bara leo.

Simba inaivaa African Lyon katika mechi muhimu ya Ligi Kuu Bara hasa kwa Simba ambao wanataka ubingwa.

Lyon watakuwa wanaiihitaji mechi hiyo kama sehemu ya ushindi ili kujihakikishia kubaki ligi kuu.

“Kocha ametuambia kutokuwa na hofu au presha sana, badala yake tucheze soka katika uwezo wetu. Unajua Lyon ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kutufunga kwenye ligi,” alisema mmoja wa wachezaji wa Simba ambao ni wazoefu.

“Utaona hata katika kombe la shirikisho hatukucheza katika kiwango kizuri sana maana ilikuwa ni lazima tuwafunge na wasitufunge mara ya pili.


“Ndiyo maana kocha amesisitiza sana suala la kutulia ili tucheze mpira katika kiwango chetu.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV