May 7, 2017Saul 'Canelo' Alvarez ameonyesha ni mtu wa aina nyingi kabisa baada ya kushinda pambano lake dhidi ya Julio Cesar Chavez.

Mabondia hao wote kutoka Mexico, kila mmoja alikuwa akitamba ni zaidi ya mwenzake na kilichotakiwa ni kumaliza ubishi.


Hata hivyo ilikuwa ni vigumu Chavez kumzuia Canelo ambaye alitamba kwa raundi zote 12 za pambano hilo.

Kwa ushindi huo, sasa Canelo anakwenda kuzichapa na Gennady Golovkin anayeaminika ndiye mkali zaidi katika kipindi hiki.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV