May 9, 2017

MAXIME


Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema wanachotaka dhidi Yanga leo ni kuhakikisha wanashinda mechi yao.

Yanga itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar katika mechi ya lala salama ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.

Kagera itakuwa inashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 2-6 katika mechi ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Yanga ambayo ilikuwa ni mechi ya mwisho ya Kocha Hans van Der Pluijm kuinoa Yanga akiwa kocha mkuu.

"Mechi ya Jumanne (leo) ni nyingine kabisa, hii si mechi ya Kaitaba. Kama unaona baada ya mechi ile dhidi ya Yanga haijawahi kusikia tumefungwa vile au vyovyote.

"Tunaweza kujifunza kulingana na makosa. Leo tunaiangalia mechi hii kama mechi mpya ambayo ina mipango au plani mpya," alisema.

Tayari Yanga kupitia kocha wake msaidizi, Juma Mwambusi imesema haiwezi kuibeza Kagera hata kidogo na itataka kushinda mchezo huo.

1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV