May 28, 2017


Marehemu Shose Fidelis alikuwa shabiki wa Simba hasa, ndiyo maana akaamua kufunga safari hadi Dodoma kuiunga mkono timu yake ikipambana na Mbao FC katika mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho.

Simba imefanikiwa kushinda kwa mabao 2-1 na kubeba ubingwa, lakini furaha ya Shose imeishia Dumila Morogoro baada ya kupata ajali ya gari ambalo pia lilikuwa limembeba Nahodha wa Simba, Jonas Mkude.

Katika akaunti yake ya Isntagram, inaonyesha Shose alitupia picha mbili tu jana. Ikionekana moja kabla ya mechi ya fainali na nyingine baada ya mechi hiyo.

Picha baada ya mechi anaonekana akiwa na Meneja wa Simba, Mussa Mgosi na mashabiki wengine wa Simba.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV