May 12, 2017


Unaweza kusema kile ambacho tulikuwa tukikuandikia kwamba kinakuja, sasa ni rasmi.


Kampuni ya kubashiri ya SportPesa tayari ni wadhamini rasmi wa Simba. Wameingia mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya jumla ya Sh bilioni 4.9.

Huu unakuwa ni udhamini mkubwa zaidi kwa Simba kuwahi kupata. Leo rasmi Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa SportPesa, Pavel Slavkov alimkabidhi Rais wa Simba, Evans Aveva jezi yenye nembo ya kampuni hiyo kifuani.

Hii inaiondoa Simba kwenye hasara ya msimu mzima. Kwani ilikuwa ikicheza bila ya kuwa na mdhamini baada ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kutotaka kuendelea.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV