Simba inaanza rasmi udhamini wake na kampuni ya michezo ya kubahatisha au kubashiri ya SportPesa.
SportPesa kutoka Kenya watatangaza udhamini huo rasmi leo na katika mechi kati ya Simba dhidi ya Stand United inayoendelea, Simba wameanza na jezi ambazo hazina mdhamini kama ambavyo imekuwa kwa msimu wote.
Lakini imeelezwa, kipindi cha pili watabadilisha na kuvaa rasmi zenye nembo ya mdhamini wao mpya SportPesa.
Kuvaa kwa Simba jezi hizo, itakuwa ni rasmi safari na mdhamini huyo kuanza.
SportPesa inasifiwa kusababisha mabadiliko katika soka la Kenya ktokana na udhamini wao kuwa juu.
0 COMMENTS:
Post a Comment